Wizara ya Fedha yaomba kuidhinishwa Sh tril 15

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba.

Wizara ya Fedha na Mipango imeomba ridhaa ya Bunge kuidhinisha Sh trilioni 15.94 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Sh trilioni 15.38 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh bilioni 564.22 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, leo amewasilisha bungeni bajeti ya wizara hiyo makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Advertisement