Mbwa wa Rais wapotea Malawi

POLISI nchini Malawi wanachunguza wizi wa mbwa wanne wa polisi waliopotea kutoka Ikulu ya Rais mjini Lilongwe wakati wa mpito wa kisiasa mwezi Septemba. Taarifa kutoka Ikulu ya Malawi zinaeleza kuwa Godfrey Arthur Jalale, aliyekuwa kiongozi wa wafanyakazi wa Ikulu chini ya Rais wa zamani Lazarus Chakwera, amekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Mbwa hao, aina ya German Shepherd, wanadaiwa kuwa na thamani ya dola za Marekani 2,300 (takriban Sh. 6.4 milioni), na walitolewa nje ya jumba hilo kati ya Septemba 19 na Oktoba 4, kulingana na waendesha mashtaka. Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hili, ambalo limeibua wasiwasi mkubwa katika vyombo vya usalama nchini humo. SOMA: Namna ya kufanya mbwa asile chakula cha adui

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button