Wrrb yatoa mafunzo mfumo wa stakabadhi za Ghala

DAR ES SALAAM: Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imetoa mafunzo ya utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi za ghala kama ilivyo utaratibu wake wa kila mwaka kwa Watendaji  wa kampuni za Waendesha ghala,  Wasimamizi wa ghala,  Meneja dhamana  pamoja na washiriki binafsi.

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkuu wa  wilaya ya Ubungo Hashim Komba katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo katika Uwanja wa  Maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa  Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Mafunzo hayo, Komba alieleza kuwa  Mafunzo haya yanakwenda kuongeza heshima kwa watendaji wa ghala na kupelekea utoaji wa huduma bora kwa  Wadau wote, vilevile ameitaka WRRB kuongeza matumizi ya TEHAMA katika utendaji ili kuendana na mabadiliko ya dunia.

Pia, mafunzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB Asangye Bangu pamoja  na  Mkurugenzi wa huduma za uendeshaji  wa Biashara kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Mary Fidelis.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Stakabadhi  za Ghala Asangye Bangu amesema kuwa  lengo kubwa ni kuongeza tija katika ufanyaji kazi na matarajio ya mafunzo  hayo ni kuhakikisha kazi zinafanywa  kwa usahihi kwa kuzingatia sheria .

Aidha Bangu ameongeza kuwa Bodi ya Udhibiti na Usimamizi wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala imejipanga kuona ambavyo watatekeleza shughuli zao za kiserikali pia wamejitaidi kuingiza bidhaa mbalimbali kadiri sheria ilivyo waruhusu kufanya  hivyo, Washiriki  waliojitokeza kupata mafunzo haya  watapatiwa cheti cha kufuzu usimamizi wa shughuli za uendeshaji ghala  ambacho  kitatambuliwa na  Bodi ya Stakabadhi za Ghala.

‘’nilipofanya ukaguzi nilibaini changamoto mbalimbali  kwenye maghala, anaeshikiliwa kwanza ni Meneja na Mkurugenzi anakuwa hayupo ukimuuliza  Mkurugenzi anakuambia Meneja wangu ndio anaehusika, kwahiyo mda mwingine unakuta meneja hana Taarifa, hivyo natoa wito kwa Washiriki wote kuzingatia Mafunzo yanayotolewa ili kuwaongezea uwezo wa Kiutendaji” Amesema Bangu.

Habari Zifananazo

Back to top button