LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea kushika kasi, huku leo viwanja vitatu vikitarajiwa kuwaka moto.
Bingwa mtetezi Yanga itakuwa uwanja Azam Complex, Dar es Salaam kuikaribisha Pamba Jiji.
Yanga ipo nafasi ya 4 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 9 baada ya michezo 4 wakati Pamba Jiji inashika nafasi ya 14 ikiwa pointi 4 baada ya michezo 6.
SOMA: Ken Gold mikononi mwa Yanga Ligi Kuu leo
Huko Lindi, Azam itakuwa mgeni wa Namungo kwenye uwanja wa Majaliwa ulipo Ruangwa.
Azam inashika nafasi ya 5 ikiwa na pointi 9 baada ya michezo 6 wakati Namungo ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 6 baada ya michezo 5.
Eneo la Mwenge, Dar es Salaam litakuwa na hekaheka wakati wenyeji KMC itakapoikaribisha Kagera Sugar kwenye uwanja wake wa KMC Complex.
Katika msimamo wa ligi KMC ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 6 wakati Kagera Sugar ni ya 15 ikiwa na pointi 4.