Yanga kuzindua Yang Z Jumamosi
YANGA inatarajia kuzindua tawi la vijana lenye washiriki 500 maarufu kama Yang Z kwenye fukwe za Upepo Mbezi beach, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam Leo Msemaji wa Yanga Ally Kamwe amesema uzinduzi huo utakaofanyika Jumamosi ya wiki hii utaenda sambamba na sherehe ambapo kutakuwa na vinywaji, vyakula na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa muziki.
SOMA: Yanga ni kama maji haikwepeki
Uzinduzi huo unakuja baada ya Kamwe kuhamasisha vijana wenye umri kuanzia miaka 20-35 kulipia ad ash 29,000 na kujiunga na kundi hilo ili kuwa sehemu ya washiriki 500 wa tawi hilo jipya.
Kamwe ametumia wiki tatu katika uhamasishaji na kupata mwitikio mzuri wa vijana hao ambao watakabidhiwa rasmi kadi zao za uanachama wa klabu hiyo.
SOMA: Yanga ni kama maji haikwepeki
“Kwa vijana wanaotaka kuja kuungana na wenzao nab ado hajajiunga waje n ash 29,000 watoe fedha watapewa na kadi na kuingia ndani, milango bado iko wazi,”amesema.
Amesema washiriki wote watatumiwa meseji za mialiko zitakazokuwa kama kadi ya kuingilia kwenye fukwe hizo.
baada ya kusherehekea amesema wataweka mipango ya namna ya kuendesha tawi hilo la vijana.
Mwisho