Yanga kwenye ramani ya robo fainali CAFCL

DAR ES SALAAM: Mabingwa wa kandanda nchini Yanga, leo wanakibarua kizito katika Uwanja wa Benjamini Mkapa wakiwa wenyeji wa CR Belouizdad ya Algeria.
Huu ni mchezo wa tano kwa timu hizo katika kundi D la michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Timu zote mbili zinautizama mchezo huo kama tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika, mpaka sasa Yanga na Belouizdad wana alama tano katika kundi D kitu kinachokoleza ugumu wa mchezo wa leo usiku.
Ikiwa Yanga watashinda mchezo huo watajiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya robo fainali kwani watafikisha alama 8 na hivyo kuhitaji alama moja tu katika mchezo wa mwisho ili kujikatia tiketi ya kufuzu.