Yanga, Simba ng’adu kwa ng’adu kileleni

MBEYA:  MBIO za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2025/26 kati ya Yanga na Simba zinazidi kunoga na lugha rahisi unayoweza kusema vita yao ni ng’adu kwa ng’adu kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Leo miamba hiyo yote ilikuwa ugenini, ambapo Yanga ilikuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya ikicheza dhidi ya Prisons na kuibuka na ushindi wa mabao  0-5 huku Simba pia ikiwa ugenini Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora iliibuka na ushindi kama huo.

Kutokana na ushindi huo Yanga imefikisha pointi 76 kwa michezo 28, huku Simba nayo ikifikisha pointio 75 kwa michezo kama hiyo ya Yanga.

Timu hizo zote zimebakikisha mechi mbili, ambapo  Jumapili wiki hii Simba itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar, huku Yanga ikiikaribisha Dodoma Jiji. Kisha Jumatano Juni 25, 2025 zitakutana zenyewe mechi yao ya kiporo iliyokuwa ichezwe Machi 8, 2025.

Azam nayo inashika nafasi ya tatu, huku leo ikipata ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Tabora United kwenye Uwanja wa Azam Complex na imefikisha pointi 60 ikiwa na mechi moja mkononi.

Matokeo ya michezo mingine leo:

Pamba 1-0 JKT Tanzania

Mashujaa 1-1 KMC

Dodoma 1-2 Singida

Coastal 1-0 Fountain Gate

Namungo 0-0 Kagera Sugar

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button