Yanga, Simba viwanja tofauti Ligi Kuu wanawake leo

MECHI nne za raundi ya tatu Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara zinapigwa leo viwanja tofauti.

Bingwa mtetezi Simba Queens ipo ugenini dhidi ya Ceasiaa Queens kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.

SOMA: Ligi Kuu wanawake kuanza kutimua vumbi leo

Advertisement

Yanga Princess itakuwa uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam kuikaribisha Mashujaa Queens.

Miamba mingine ya soka la wanawake, JKT Queens itashuka uwanja wake wa nyumbani wa Maj Gen Isamuhyo kuialika Mlandizi Queens.

Bunda Queens ya Musoma mkoani Mara itakuwa mgeni wa Gets Program kwenye uwanja wa Kituo cha Ufundi cha TFF, Kigamboni, Dar es Salaam.