Yanga watoa pole waathirika mafuriko Hanang

UONGOZI wa klabu ya Yanga umetoa pole kwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea eneo la Katesh Wilaya ya Hanang mkoani Manyara jana.

“Mwenyezi Mungu azilaze mahala pema roho za marehemu waliofariki katika mafuriko hayo na tunawaomba majeruhi wote wapone haraka.” imeeleza taarifa yao.

Aidha mapema leo taarifa ya Ikulu imeeleza hadi sasa idadi ya vifo ni 50 huku idadi ya majeruhi waliowasilishwa katika hospitali mbalimbali za mkoa, wilaya na vituo vya afya ni zaidi ya 80.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa kaya zilizoharibiwa hadi sasa ni 1,150 idadi ya watu walioathirika ni 5,600 na takribani ekari za mashamba 750 zimeharibiwa.

Habari Zifananazo

Back to top button