Yanga yaitandika Vital’O

DAR ES SALAAM: KLABU ya Yanga imepita hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao wa mabao 6-0 dhidi ya Vital’o mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, jijini.

Baada ya ushindi huo Yanga wanachukua jumla ya Million 30 za kitanzania kupiti’ goli la Mama’ fedha ambazo zinatolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa timu inayofunga bao katika mashindano ya kimataifa

Mabao ya Yanga kwenye mchezo huo yalifungwa na Pacome Zouzoua dakika ya 13 penalti baada ya beki wa Vital’O, Amedee Ndavyutse kucheza mpira kwa mkono katika harakati za kuokoa mpira katika eneo la 18 kipa wake Hussein Nyashimiye kutoka kwenye eneo lake.

SOMA: Yanga ni kama maji haikwepeki

Yanga waliongeza bao la pili dakika ya 48 lililowekwa kimiani na Clement Mzize akimalizia kwa shuti mpira pasi kutoka kwa Stephen Aziz Ki amechukuwa nafasi ya Aziz Andambwile bao la tatu limefungwa na Chama dakika ya 50.

dakika ya 71 .bao la nne lililowekwa kimiani na Prince Dube baada ya kupiga shuti na kutinga nyavuni akipokea pasi ya Chama na dakika 78, bao la tano lililowekwa kimiani na Aziz Ki baada ya kupokea pasi kutoa Chama.

Wananchi ilihitimisha Karam ya mabao dakika ya 88 bao la sita lililowekwa kimiani na Mudathir Yahya akipokea pasi kutoka kwa Clatous Chama ikiwa na Assist yake ya tatu katika mchezo huo.

Huu unakuwa ushindi wa pili kwa Yanga katika michuano hiyo ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mechi ya kwanza kushinda mabao 4-0 jumla ya mabao 8-0

Dakika ya 45 kipindi cha kwanza Yanga 1-0 dhidi ya Vital’o. Timu zote zilicheza vizuri Yanga walifamikiwa kufika langoni kwa mpinzani mara kwa mara.

SOMA: Yanga yaipania Vital’ O mchezo wa marudiano CAF

Mashambulizi ya Yanga , dakika ya 34, Clatous Chama amefanya kazi nzuri kwa kutoa pasi na mpira kumfikia Ahoua ambaye alipiga shuti na mpira kugonga mwamba.

Muamuzi wa mchezo huo Lamin Jammeh kutoka Gambia amempa kadi nyekundu Ndavyutse kwa kosa la kuucheza mpira kwa mkono ndani ya 18, dakika ya 12..

Kikosi cha Yanga: Djigui Diarra, Azizi Andambwile/ Stephen Aziz Ki, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Jonas Mkude, Duke Abuya/ Max Nzengeli, Kennedy Musonda/ Mudathir Yahya, Nickson Kibabage, Clement Mzize/ Prince Dube, Clatous Chama na Pacome Zouzoua /Aboubakar Salum.

Vital’O : Hussein Nyashimiye, Amedee Ndavyutse, Abdul Karim, Claude Masiri, Hussein Ibrahim, Kessy Jordan, Yakubu Awimana, Amiss Leon, Autriche Nsanzama, Hamis Harerimana na Prince Michel.

Habari Zifananazo

Back to top button