Yanga yaizima Prisons kikatili

DAR ES SALAAM; YANGA leo imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa KMC, Kinondoni, Dar es Salaam.

Kutokana na matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 33 ikiwa nyuma ya Simba inayoongoza ligi ikiwa na pointi 34. Yanga na Azam zote zina pointi 33, isipokuwa Yanga ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Clement Mzize, IbrahimΒ Abdullah ‘Baka’ aliyefunga mawili na Prince Dube.



