YANGA imekubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa CR Belouizdad katika mchezo wa kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa usiku huu Algeria.
–
Yanga imeruhusu bao la kwanza dakika ya 10 lililofungwa na kiungo Abdelraouf Benguit, kabla ya dakika ya 45 kiungo Abderrahmane Meziane kufunga bao la pili na dakika ya 90 Lamine Jallow kufunga hesabu.
–
Mchezo huo wa kundi D unajumuisha timu za Al-Ahly, Yanga, Belouizdad na Medeama.
–
Yanga itarudiana na timu hiyo baada ya kumaliza raundi ya kwanza ya michezo yote mitatu.


1 comments