ZAIDI ya wakazi 2,000 wa kijiji cha Maparawe kata ya Mchahuru wilayani Masasi mkoani Mtwara watanufaika na mradi wa ujenzi wa zahanati uliyogharimu zaidi ya Sh milioni 75.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zahanati hiyo, mwenyekiti wa kijiji hicho, Hashimu Saidi amesema mradi huo umewarahisishia wakazi hao kupata huduma hiyo ya afya kwa karibu zaidi muda wote.
Uzinduzi wa mradi huo umefanywa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Stergomena Tax akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani Mtwara kuhusu kuzindua na kuweka jiwe la msingi miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara.
SOMA: Wapongeza ujenzi wa Zahanati Mkomo
Kabla ya mradi wakazi wa kijiji hicho walikuwa wakitembea umbali mrefu wa takribani kilometa 10 kwenda vijiji jirani kufata huduma hiyo.
“Kwahiyo tunashukuru sana kupata huu mradi ambao umewaondolea changamoto ya muda mrefu wakazi wa kijiji hiki na maeneo jirani kuhusu suala la matibabu lakini sasa tunauhakika wa kupata huduma hii kwa urahisi mkubwa,” amesema Waziri Tax.
Mkazi wa kijiji hicho, Haruna Awadhi amesema: “Tumefurahi sasa mama Samia kutuletea mradi huu wa zahanati kwasababu umeturahisishia kwenda vijiji jirani kufata huduma ya zahanati, tulikuwa tunateseka sana tulikuwa tunaenda vijiji jirani kama vile sindano na hadi kufikia hatua hii tunashukuru sana.”
Aidha zahanati hiyo inatoa huduma mbalimbali ikiwemo ya akina mama wajawazito, wagonjwa wa nje na zingine.
Mradi huo utawanufaisha wananchi wa kijiji hicho na vingine jirani kwa kuwasogezea huduma ya afya karibu, kupunguza vifo na kuongeza tija katika ukuzaji wa uchumi ambapo zaidi ya wakazi 4,000 katika maeneo hayo watanufaika na mradi huo.
SOMA: Vijiji Newala kunufaika ujenzi zahanati
Kwa upande wake waziri huyo ameendelea kuwasisitiza wakazi wa maeneo hayo kuitumia kikamilifu? na kuitunza zahanati hiyo. Hata hivyo waziri huyo ameahidi kutoa Sh milioni 2 kwa ajili ya kujenga eneo la wagonjwa kusuburi kupata huduma kwenye zahanati hiyo.