Zaidi ya wagonjwa 1,500 kutoka nje wanatibiwa Muhimbili

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili ndio kubwa Tanzania yenye wataalamu bingwa wa kada nyingi inaelezwa kupokea wagonjwa wa nje kati ya 1,500 hadi 2,000 kwa siku, huku ikilaza wagonjwa wanaokadiriwa kufikia 1,300 huku asilimia 36 ya wagonjwa hao wakiwa ni wa msamaha.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi wakati akipokea msaada wa Luninga 10 na kueleza kuwa hiyo ni moja ya tiba kwa baadhiya wagonjwa.

Prof. Janabi amesema msaada huo ni wa manufaa kwa Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwa pesa ambazo zingetumika kununulia luninga hizo zitaelekezwa kwenye mahitaji mengine ya wagonjwa ikiwemo ununuzi wa dawa.

Advertisement

Luninga hizo zimetolewa na Kampuni ya Bima ya Assemble Insurance (T) Ltd ikiwa ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo kurejesha kwa jamii hivyo pia itasaidia kuhabarisha ndugu wanaouguza wagonjwa hospitalini hapo.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Assemble, Tabia Massoud amesema, kampuni yake inavutiwa kwa namna Hospitali hiyo ya Taifa inavyopiga hatua katika kuboresha huduma.

“Muhimbili ni mshirika wetu mkubwa kwa kuwa wateja wetu wengi wanahudumiwa hapa, msaada huu utawanufaisha pia na wateja wetu ambao wananufaika na huduma za matibabu hapa,” amesema Tabia Massoud.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *