Zaidi ya watu 35 wauawa Ituri DRC

CONGO: WANAMGAMBO wenye silaha wamewaua zaidi ya raia 35 na kuwajeruhi wengine kadhaa katika shambulio lililotokea usiku wa Jumatatu katika vijiji vya jimbo la Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kiongozi wa kundi la Djaiba katika vijiji vya Djugu, Jean Vianney, amesema wanamgambo wa CODECO walitekeleza shambulizi hilo lililozuka majira ya saa mbili usiku, wakiwauwa wakaazi kwa risasi na kuteketeza nyumba zao kwa moto.

Vianney alisema, “Tumewahesabu zaidi ya watu 35 waliokufa majira ya asubuhi hii leo, na juhudi za kutafuta wahanga zinaendelea.”

Aliongeza kwamba baadhi ya watu wamejeruhiwa vibaya, na wengi wamekufa kutokana na kuungua na moto walipokuwa ndani ya nyumba zao.

Kwa upande mwingine, kiongozi wa asasi za kiraia katika eneo hilo, Jules Tsuba, amesema miili 49 ilipatikana hadi asubuhi ya leo Jumanne, huku juhudi za kutafuta waathirika zaidi zikiendelea.

CODECO ni mojawapo ya makundi mengi ya wanamgambo yanayopigania ardhi na rasilimali mashariki mwa Congo. SOMA: Malawi kuondoa Jeshi lake Congo

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button