Zambia yakamata kilo 550 za pembe za ndovu

LUSAKA: Mamlaka za Zambia zimekamata karibu kilo 550 za pembe za ndovu na kuwakamata watu tisa wanaodaiwa kuhusika na mtandao wa kimataifa wa magendo ya wanyamapori.
Operesheni hiyo ilifanyika Machi 9 jijini Lusaka baada ya taarifa za kijasusi kutoka Shirika la Environmental Investigation Agency (EIA) lenye makao yake London. Waliohifadhiwa ni raia wa Zambia pamoja na mtu mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Maafisa wa Idara ya Hifadhi za Taifa na Wanyamapori (DNPW) walivamia nyumba moja ambako walikuta shehena hiyo ya pembe za ndovu, pamoja na nyingine iliyokamatwa katika operesheni iliyofuata.
Kwa mujibu wa EIA, operesheni hiyo imehitimisha uchunguzi wa miezi kadhaa na kuvuruga mtandao unaodaiwa kufanya biashara ya pembe za ndovu katika ukanda wa Kusini mwa Afrika kwa muda mrefu.
Mkurugenzi Mtendaji wa EIA, Mary Rice, alisema hatua hiyo inaonyesha umuhimu wa operesheni zinazoongozwa na taarifa za kijasusi katika kupambana na uhalifu wa kimataifa.
Aliongeza kuwa mitandao hiyo hutumia udhaifu wa mifumo ya usimamizi na rushwa kuendesha shughuli zake, ikiwa ni pamoja na kuandaa uwindaji haramu katika nchi jirani kama Botswana na kusafirisha pembe hizo kupitia nchi kama Namibia na Angola.
EIA imesema itaendelea kufuatilia hatua za kisheria dhidi ya washukiwa hao.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com