Zanzibar kuwasilisha bajeti ya tril 4/

Zanzibar

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya Salum anatarajiwa kuwasilisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 20242025 ambayo inatarajiwa kufi kia Sh trilioni 4.08. Bajeti hiyo ni sawa na ongezeko la Sh trilioni 1.24 ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2023-2024 ya Sh trilioni 2.84.

Akizungumza wakati akiwasilisha mpango wa serikali na mwelekeo wa bajeti ya Serikali ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2024-2025, Dk Mkuya alisema ongezeko la bajeti hiyo limejikita moja kwa moja katika kutekeleza miradi ya kimkakati ambayo imepewa kipaumbele cha kwanza.

Aliitaja miradi hiyo ambayo imepewa kipaumbele cha kwanza ni pamoja na ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Pemba ambapo maandalizi yake yamekamilika ikiwa ni juhudi za kukifungua kisiwa cha Pemba kiuchumi na uwekezaji.

Advertisement

“Bajeti ya Serikali ya Zanzibar ya mwaka 2024-2025 imejikita moja kwa moja katika kutekeleza miradi ya kimkakati ambayo ni ujenzi wa uwanja wa ndege wa Pemba pamoja na bandari zilizopo Unguja na Pemba katika kuimarisha miundombinu,” alisema.

Aidha, alisema katika bajeti hiyo serikali ina matumaini makubwa ya kutekeleza miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa hospitali ya rufaa ya kibingwa inayotarajiwa kujengwa huko Binguni, Wilaya ya Kati Unguja ambapo makubaliano ya ujenzi wake yametiwa saini Korea ya Kusini hivi karibuni katika ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan.

“Matarajio yetu makubwa kuona kwamba utekelezaji wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2024-2025 ambayo tunaiita bajeti ya kimkakati imelenga zaidi kuimarisha miundombinu ya barabara, kiwanja cha ndege pamoja na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Pemba,’’ alisema.