Zanzibar mwenyeji Mkutano wa 20 wa Benki ya Dunia

ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania Nathan Balete na ujumbe wake Ikulu Zanzibar leo tarehe 27 Oktoba 2023.
Katika mazungumzo yao wamegusia ushirikiano uliopo kati ya Benki ya Dunia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo uchumi wa buluu , sekta ya nishati hususani umeme wa jua, upepo na suala la gesi asilia, elimu, afya, kilimo, kujenga uwezo na msaada wa kiufundi, uwezeshaji wa Wanawake, Mahakama na mengineyo.
Aidha Rais Dk.Mwinyi ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuisaidia Zanzibar katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Naye Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Dk.

Saada Mkuya amesema Zanzibar itakuwa mwenyeji wa mkutano wa 20 wa mapitio wa Benki ya Dunia utakaoshirikisha wajumbe 350 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga kuanzia tarehe 06 hadi 08 Disemba mwaka huu katika Hoteli ya Golden Tulip Airpot Mkoa wa Mjini Magharibi.
Advertisement

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *