Rais Mwinyi aongoza mazishi ya Ali Ameir

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza Viongozi na Wananchi katika mazishi ya Mwanasiasa Mkongwe, Marehemu Ali Ameir Muhammed, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo, tarehe 26 Novemba 2025.

Marehemu Ali Ameir alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam. Mapema kabla ya mazishi, Rais Dk. Mwinyi alijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Jeneza iliyoswaliwa katika Msikiti wa Donge Kichamvyaani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, ambako pia alitoa mkono wa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu.

Marehemu Ali Ameir alikuwa kiongozi mwenye historia ndefu katika utumishi wa umma. Aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, ikiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbunge wa Jimbo la Donge, Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, pamoja na Mhariri wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo. Alikuwa pia Mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa CCM Taifa. SOMA: SMZ yajipanga kuzuia usafirishaji wa binadamu

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button