DAR ES SALAAM: Mfanyabiashara Zari Hassan kesho anatarajia kwenda kuwatembelea wazazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kugawa nepi za watoto ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongeza mkataba na kampuni ya Softcare ili kuendelea kuzitangaza bidhaa za kampuni hiyo amesema
“Kwa kuanza katika majukumu yangu kesho nitatembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili ili nikawape zawadi wazazi na watoto kama sehemu ya kurudisha kwa jamii.” Amesema Zari