Zarif aomba kujiuzulu kufuiatia shinikizo la wanasiasa

TEHRAN : MAKAMU wa Rais wa Iran, Mohammed Javad Zarif, amewasilisha barua ya kujiuzulu, hatua inayotafsiriwa kama ishara ya kusalimu amri mbele ya shinikizo kutoka kwa wanasiasa wa misimamo mikali nchini Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran (IRNA), Zarif amewasilisha barua hiyo kwa Rais Masoud Pezeshkian. Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Zarif kutangaza kujiuzulu, ingawa haikufahamika awali kama Rais Pezeshkian alikubali ombi hilo.

Zarif, ambaye alikuwa na jukumu kubwa katika mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 kati ya Iran na madola yenye nguvu, alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje, amekuwa akilengwa kwa muda mrefu na wanasiasa wa Iran, hasa kutoka kwenye mfumo wa kidini unaotawala nchi hiyo.

Wanasiasa hao wanamlaumu Zarif kwa ushauri wake wa kutaka kujenga mahusiano ya karibu na Marekani.

Soma: Tupo tayari kufanya mazungumzo- Iran

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button