Zelensky apongeza kusimamishwa usafirishaji gesi ya Urusi

UKRAINE : RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amepongeza kusimamishwa kwa usafirishaji wa gesi kutoka Urusi kupitia nchi yake kwenda mataifa ya Ulaya.

Zelensky amesema hatua hii ni dalili ya kushindwa kwa Moscow katikati ya uvamizi wake unaoendelea, ambao umedumu kwa karibu miaka mitatu.

Usambazaji wa gesi ya Urusi kwa mataifa ya Ulaya kupitia Ukraine ulisimama jana, baada ya Zelensky kukataa kuendelea na mkataba wa ushirikiano wa miongo kadhaa ambao umekuwa na manufaa kwa pande zote mbili.

Advertisement

Rais Zelensky alimtuhumu moja kwa moja Rais Vladimir Putin wa Urusi kwa kuvunjika kwa ushirikiano huo.

SOMA: Urusi Ukraine wabadilishana mamia ya wafungwa

Aidha, Ukraine ilizishambulia nchi ambazo bado zinanunua gesi kutoka Urusi, ikisema kuwa zinasaidia Moscow kwa kutoa mapato yanayotumiwa kuendesha vita vyake.

Kwa upande mwingine, Urusi imesema kwamba Ukraine inajiongezea matatizo kwa kushinikiza kusitishwa kwa usafirishaji wa gesi na kuwatia shaka washirika wake wa Ulaya Mashariki, ambao wanategemea usambazaji wa gesi kutoka Urusi.