Zelenskyy kukutana na viongozi wa Ulaya

RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema bado kuna uwezekano wa kurekebisha uhusiano wake na Marekani, baada ya majibizano makali na Rais Donald Trump katika Ikulu ya White House Ijumaa jioni.

Zelensky ameyasema hayo alipohojiwa na kituo cha Fox News na kuongeza kuwa Ukraine inahitaji mno msaada wa Marekani ili kupambana na Jeshi la Urusi alilolitaja kuwa na uwezo mkubwa wa wanajeshi na silaha bora zaidi.

Hata hivyo, Zelensky amekataa kuomba msamaha akisema hadhani kuwa hajafanya kosa lolote.

Wakati hayo yakiendelea leo, Zelenskyy anatarajia kukutana na kufanya mkutano na viongozi wa Ulaya.

Mkutano huo unakuja siku moja baada ya kiongozi huyo kuondoka Ikulu ya Marekani bila kutia saini mkataba wa madini baada ya kuzuka zogo baina yake na Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

Jana, Zelenskyy alitarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer kabla ya mkutano wa leo.

Viongozi wa Ulaya wamemuunga mkono, Zelenskyy baada ya mabishano makali na Trump wakisema kuwa, Zelenskyy ameonesha uhodari katika kusimama na watu wake wa Ukraine.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button