Zimbabwe, Botswana kusafiri bila pasipoti

MATAIFA ya Zimbabwe na Botswana yanafanyia kazi mpango wa kufuta mahitaji ya hati ya kusafiria ‘pasipoti’ kwa raia wa nchi zingine.

Hatua hiyo ni katika kuungana na baadhi ya nchi Afrika kupunguza vizuizi vya kuingia wageni kutoka katika baadhi ya nchi.

“Sisi wawili tumekubaliana kwa sababu sisi ni Waafrika.

Advertisement

Tunapaswa kuingia Botswana, kuingia Zambia, kuingia Kenya. Kwa nini tujizuie?” Rais wa Zimbabwe Emmerson alisema.

“Tunajiwekea vikwazo sisi wenyewe ambao ni wakoloni kuliko wao wazalendo, hivyo tukakubaliana kuwa Rais Masisi mwenyewe kwa upande wake na mimi kwa upande wangu tunakwenda kuziagiza idara husika kupunguza vikwazo hivi vya watu kusafiri kati ya nchi zetu mbili”. ameongeza.

2 comments

Comments are closed.