ZIPA: Mkutano uwekezaji utahamasisha fursa uwekezaji

MAMLAKA ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imesema Mkutano wa Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar unalenga kuhamasisha fursa mpya za uwekezaji katika sekta mbalimbali visiwani humo.

Mkutano huo wenye kaulimbiu isemayo ‘Ni Wakati wa Pemba 2025’ utafanyika katika Kisiwa cha Pemba kuanzia Mei 7 hadi 10, mwaka huu huku.

Pemba inapewa kipaumbele kama eneo jipya lenye uwezo mkubwa wa kuvutia vitega uchumi vya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Aprili18,2025, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Saleh Saad Mohamed amesema mkutano huo ni sehemu ya utekelezaji wa dira ya maendeleo ya Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi, inayotilia mkazo maendeleo jumuishi na ustawi wa kiuchumi wa kisiwa hicho.

Amesema sekta zitakazopewa kipaumbele katika mkutano huo ni pamoja na uchumi wa bluu, kilimo, utalii, nishati mbadala, na viwanda vya uzalishaji bidhaa huku wadau mbalimbali wakiwemo wajasiriamali, mashirika ya maendeleo, na taasisi za serikali yakihimizwa kushiriki.

“Tunalenga kujenga uchumi shirikishi unaozingatia uwazi, ushirikiano na mazingira rafiki kwa wawekezaji hivyo huu ni wakati sahihi kwa kila mmoja kuja na kuwa sehemu ya mabadiliko ya kweli kwa Pemba,” amesema Saad.

Kwa mujibu wa ZIPA, zaidi ya washiriki 750 kutoka sekta mbalimbali wanatarajiwa kushiriki, wakiwemo wakurugenzi wakuu wa makampuni, wawekezaji wa kimataifa, viongozi wa serikali na wanadiplomasia. Mkutano huo utajumuisha mijadala ya hali ya juu, maonyesho ya biashara ya siku mbili, ziara za kijamii, pamoja na hafla ya wawekezaji itakayoandaliwa na Rais Dk Mwinyi.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I’m getting 88 D0llars consistently to deal with net. Q I’ve never accepted like it tends to be reachable anyway one of my most noteworthy buddy got D0llars 27,000 D0llars in three weeks working this basic task and she impacted me to avail…
    Take A Look Here….> https://Www.earnapp1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button