Watafiti wabaini teknolojia rahisi ya upandaji wa pamba

MKULIMA wa pamba kutoka Kata ya Nkoma wilayani Meatu mkoani Simiyu, Shoga Fares anaelezea jinsi alivyopata elimu ya kilimo bora kwa kulima eneo dogo linalompatia mavuno mengi.

Fares anaeleza hayo wakati akizungumza na HabariLEO kuhusu historia yake katika kilimo cha pamba huku akikiri linampatia faida. Anaeleza alianza kulima pamba mwaka 1985 wakati huo akilima ekari 20 zilizompatia tani nane mpaka 10 kwa maana ya wastani wa kilo 500 kwa ekari.

Fares anasema baadaye alianza kutumia mbegu za kisasa baada ya kupata elimu kutoka kwa watafiti mbalimbali wakiwemo wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kituo cha Ukiliguru mkoani Mwanza.

“Ushauri walionipa ni kupunguza eka nilizokuwa nikilima na kulima eka chache ili nizihudumie na kupata mavuno mengi. Nimefuata ushauri wao umeleta tija katika kilimo changu,” anasema Fares. Anasema mwaka huu 2022/2023 amelima eka sita amepata mavuno kilo 3,200 ambayo ni sawa na tani tatu.

“Nawashauri wakulima walime kilimo cha tija bila kuchanganya pamba na mazao mengine. Wafuate ushauri wa wataalamu wa kulima kisasa ili wapate kilo nyingi kwa ekari moja,” anasema.

Wakati Fares akitoa ushauri kwa wakulima wenzake, Mtafiti kutoka Tari Kituo cha Ukiliguru Mwanza, Dawson Malela anasema watafiti kituoni hapo wametafiti teknolojia ya zao la pamba ambayo itamwezesha mkulima kupanda kisasa na kutumia muda mfupi shambani.

Anasema wazo la teknolojia hiyo ya kumrahisishia mkulima kupanda lilianza Agosti mwaka jana, inawezesha wakulima kupanda mbegu sentimeta 60 kutoka mstari hadi mstari na sentimeta 30 kutoka mmea hadi mmea.

Malela anaeleza mwanzoni wakulima wa pamba walipanda zao hilo kwa nafasi ya sentimeta 90 kutoka mstari hadi mstari na sentimeta 40 kutoka mmea hadi mmea. “Sasa watafiti wakaja na teknolojia mpya ambayo ni sentimeta 60 kutoka mstari hadi mstari na sentimeta 30 kutoka mmea hadi mmea.

Kwa nini teknolojia hizi mbili za kupanda? Teknolojia ya awali ya sentimeta 90 kwa 40 ilikuwa inakuwa na mimea 22,000 kwa ekari. “Lakini ujio wa sentimeta 60 kwa 30 unamfanya mkulima kuwa na mimea 44,444 mara mbili ya nafasi ya kwanza.

Sasa changamoto iko wapi? Ni kwamba nafasi zinakuwa karibu sana kwa sentimeta 60 kwa 30 hali inayosababisha mkulima wakati mwingine kupata JADIDAAA ugumu kuchukua teknolojia hiyo mpya,” anasema Malela. Kwa kuliona hilo, watafiti kutoka kituo cha Ukiliguru walitafiti teknolojia rahisi ya kumsaidia mkulima kupanda kwa nafasi sahihi.

“Teknolojia hii sasa ina uwezo wa kuchimba mashimo yenyewe na kwa nafasi ya sentimeta 60 lakini pia inaweka mbegu kwa hatua za sentimeta 30 kutoka mmea hadi mmea. Pia teknolojia hii inafukia mbegu hizo,” anasema.

Anaeleza kwa teknolojia hiyo mkulima ana uwezo wa kuhakikisha mbegu zimepandwa kikamilifu bila kuwa na vibarua wengi, kwani inatumia saa moja kwa eneo la ekari moja na inaongozwa na mtu mmoja tu.

Anasema tofauti na wakulima walivyokuwa wakipanda eneo la ekari moja kwa kutumia jembe la mkono ambapo walitakiwa wakulima kati ya wanane mpaka tisa waliotumia muda wa saa nane mpaka tisa.

“Sasa hii ni mkombozi kwa upande wa muda kwa sababu inatumia muda wa saa moja wakati kupanda kwa jembe la mkono saa nane mpaka tisa. Lakini itasaidia kuondoa gharama za vibarua.

Wastani kwa kibarua mmoja kwa siku huwa ni shilingi 4,000, kwa hiyo ukiwa nao wanane unazungumzia shilingi 32,000 na kuendelea. “Wakati hii teknolojia ya kupandia inatumia lita moja ya petroli kwenye eneo la ekari moja. Thamani ya lita moja ni wastani wa shilingi 3,200.

Mwendeshaji ni mmoja anayelipwa shilingi 5,000. Sasa 5,000 ukijumlisha shilingi 3,000 inakuwa ni shilingi 8,000 ambayo ni gharama nafuu na inakomboa muda kwa hiyo wakati wa kupanda vibarua wakisumbua ukiwa na mashine hiyo utapanda kwa wakati na ukahakikisha msimu umeuwahi,” anasema Malela.

Kwa upande wake Mtafiti Msaidizi kutoka TARI Ukiliguru, Robert Cheleo anasema uvumbuzi wa nafasi mpya ya upandaji ulifanyika ukiongozwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Ukiliguru, Dk Paul Saidia ambaye ndiye Mratibu.

Anasema katika zao la pamba kuna teknolojia ambazo zimevumbuliwa kwa kupitia tafiti mbalimbali na moja ya teknolojia hizo ni mbegu bora za zao la pamba aina ya UKM08 ambayo imeboreshwa ina uwezo mkubwa wa kuzaa na kutoa mavuno ya kutosha ya wastani wa kilo 1,200 kwa ekari.

Lakini pia mbegu hiyo ina uwezo mkubwa wa kutoa nyuzi pamba na mbegu kwa asilimia 43. “Pia ina uwezo mkubwa wa kukabiliana na wadudu wafyonzaji na watafunaji. Aina hii ya mbegu ina manyoya katika majani yake, manyoya hayo yana uwezo mkubwa wa kutengeneza umbali kutoka kwenye nyweleo hadi kwenye ujani kiasi kwamba yule mdudu anashindwa kuathiri moja kwa moja jani.

“Kwenye jani ndiko kuna kiwanda cha kutengeneza chakula kwa njia ya jua na kupeleka katika vitumba ambapo huko ndiko kwenye lengo letu tupate vitumba vya kutosha na vyenye afya ya kutosha.

“Sasa ukiutunza vizuri mmea wa pamba vikawepo vitumba vyenye wastani wa idadi ya vitumba 10 angalau kwa kila mche, tunatarajia kuwa na wastani wa mavuno wa kilo 700 kwenye eneo la ekari moja,” anasema Robert Cheleo.

Anasema kwa kuwa wakulima wanashindwa kuhudumia vizuri shamba wengi wao wanaangukia kwenye kilo za pamba kati ya 300 hadi 400 kwa hiyo hata hiyo nafasi ya zamani bado hawakufanya vizuri. “Lakini sasa watafiti wakaona kuna haja ya kufanya utafiti kwenye nafasi ya upandaji ili mkulima alime kwa tija ndipo hapo wakaja na nafasi ya sentimeta 60 kutoka mstari hadi mstari na 30 kutoka shimo hadi shimo.

“Miche hii ni mara mbili zaidi ya nafasi ya zamani. Sasa ukilea angalau wastani ya vitumba 10 kwa kila mche tunategemea kuwa na mavuno ya kilo 1,200 hadi 1,400 kwa ekari moja,” anasema.

Anasisitiza mkulima akitunza vizuri mmea huo wa pamba anaweza kupata mavuno yatakayomsaidia kupata kipato.

Pia anasema kuna teknolojia nyingine ya kupunguza kwa kukata matawi yasiyozaa katika mmea kuusaidia uwe na machipukizi mengine mengi ambayo yana uwezo wa kuzaa matunda.

“Hata hivyo, kukishakuwa na machipukizi mengi yenye uwezo wa kuzaa matunda tunatarajia kuongeza mavuno kutoka kwenye kilo 1,200 kwa ekari hadi 4,000.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
feniko1010
feniko1010
2 months ago

Making an extra $15,000 per month from home by doing easy copy and paste type internet work. I earned $18,000 from this simple at-home job. Everyone may now easily generate additional money online.
.
Detail Her———————>>>http://www.dailypro7.com

Velma L. Thomas
Velma L. Thomas
Reply to  feniko1010
2 months ago

I’m making a decent compensation from home $60k/week , which was astonishing under a year prior I was jobless in a horrendous economy. I was honored with these guidelines and presently it’s my obligation to show sv02 kindness and share it with Everyone
.
.
Detail Are Here——————————>>> https://fastinccome.blogspot.com/

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x