Tanzania kufungua tawi nchini hospitali ya Appollo

SERIKALI ya India imekubalia ombi la Tanzania kufungua tawi la Appollo nchini ili kusogeza huduma za matibabu kwa Watanzania wengi zaidi.

Kukubaliwa kwa ombi hilo limetokana na ziara ya kitaifa nchini India iliyofanywa na Rais Samia kuanzia Oktoba 8 -11 mwaka huu kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya India, Droupadi Murmu.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa kipaumbele kikubwa cha Tanzania katika ziara hiyo ilikuwa ni dawa, ambapo kuna uhitaji mkubwa wa dawa nchini.

“Kiwango cha dawa kinachozalishwa Tanzania ni kidogo ukilinganisha na mahitaji, kwani 80% ya dawa hununuliwa nje ya nchi ambapo 60% hutoka India. Hivyo katika mazungumzo na wenzetu wa India, Tanzania imesisitiza umuhimu wa Wafamasia wa India kuzalisha humu humu nchini,” Imeeleza taarifa yake.

“Na hilo likifanikiwa ina maana hatua hiyo italinufaisha soko la Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Kusini mwa Afrika (SADC). Aidha, India na Tanzania zimekubaliana kuanzisha kituo cha tiba asilia nchini.” Imefafanua taarifa hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button