Al Ameen Foundation yasaidia watoto vifaa vya shule Dar

DAR ES SALAAM; TAASISI ya kidini ya Al Ameen Foundation ya Dar es Salaam, imefanikiwa kugawa vifaa vya shule kwa watoto wapatao 150, ikiwa ni sehemu ya kusaidia elimu, utu na matumaini wa watoto.

Hafla ya kugawa vifaa hivyo ilifanyika mwishoni mwa wiki makao makuu ya taasisi hiyo Kijitonyama kwa Ali Maua, Dar es Salaam ikiwa ni hitimisho la programu maalumu ya taasisi hiyo iitwayo Vifaa Shule 2026, ambapo wanachama wa taasisi hiyo huchangia ili kusaidia watoto wakiwemo yatima.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Ghalib Monero amesema Januari 3, 2026 walifanya hivyo kwa watoto wa madrasa Sabera iliyopo Kijiji cha Magoza, Mkuranga, Pwani na mwsihoni wa wiki walifanya hivyo Kijitonyama..

“Lilikuwa tukio kubwa zaidi ofisini kwetu Al Ameen Foundation Kijitonyama, ambapo tulitoa vifaa mbalimbali ikiwemo madafatari na kalamu kwa watoto,” amesema Monero na kuongeza kuwa taasisi yake ni ya kidini inayohusika na masuala mbalimbali ya kijamii.

Amesema hafla hiyo ilipambwa na viongozi na wanazuoni mbalimbali na kuwataja baadhi kuwa ni Sheikh Mohammed Nassor Amran (Rais wa taasisi), Sheikh Omar Mgaza (kutoka Ofisi ya Mufti Daahwa), Sheikh Dau Silima, kutoka Wakf na Mali Amana Zanzibar (Kitengo cha Zakaah na Sadaka) na Sheikh Ahmad Rajab, msomi kutoka Chuo Kikuu cha Al Azhar Shareef, Misri.

“Viongozi hawa walitoa nasaha, dua na hamasa, wakisisitiza umuhimu wa kuwalea yatima kwa misingi ya dini, elimu na maadili mema, sambamba na kushirikiana katika kazi za kheri kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu.

“Tunatoa shukrani za dhati kwa wafadhili wote, wadau, wanachama na kila aliyeshiriki kwa njia moja au nyingine kufanikisha tukio hili,” amesema Monero.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button