Wanawake kupata mafunzo ya uwekezaji Dar

DAR ES SALAAM: ZAIDI ya vikundi vya wanawake mia moja kutoka Mkoa wa Dar es salaam wanaratajiwa kupata mafunzo ya uwezeshwaji kiuchumi ili kuongeza uelewa na ubunifu.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dar es salaam, Amina Good Said ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Amo.

Amesema mafunzo hayo yatafanyika Februari 13,mwaka huu katika ukumbi wa blessing Kata ya Segerea wilayani Ilala mkoani Dar es salaam.

Katika hatua nyingine Amina ameeleza kuwa mafunzo hayo yatafunguliwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Halima Mamuya.

Amina amebainisha kuwa Mafunzo hayo yanawalenga wanawake na makundi yote ya kinamama yanayofanya shughuli za kiuchumi ili kujiongezea kipato.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button