Vijana 5,746 waanza mafunzo uanagenzi

SERIKALI imesema itaendelea kuratibu na kuimarisha sera, sheria na miongozo inayosimamia programu za mafunzo ya uanagenzi, pamoja na kuhamasisha sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kutoa nafasi za mafunzo kwa vitendo kwa wanagenzi nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu), Deus Sangu amesema hayo leo Machi 3, 2026 katika Chuo cha Ufundi Stadi cha Don Bosco jijini Dodoma wakati akifungua Awamu ya Nane ya Mafunzo ya Stadi za Kazi kwa Njia ya Uanagenzi kwa vijana 5,746 waliodahiliwa katika vyuo 46 nchini kwa mwaka wa masomo 2025/26.
Amesema utekelezaji wa programu hiyo umewezesha jumla ya wanufaika 93,495 hadi kufikia Februari 2026. Waziri Sangu amesema mafunzo hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kuwapa vijana uzoefu wa kazi kwa nadharia na vitendo, kupunguza pengo la ujuzi kati ya mafunzo ya kitaaluma na mahitaji ya waajiri, pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa vijana kuajiriwa au kujiajiri.

“Hii ni dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kujenga nguvukazi yenye ushindani na tija kwa maendeleo endelevu ya Taifa,” amesema.
Aidha, amesisitiza kuwa kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Tanzania inahitaji nguvukazi yenye ujuzi, weledi na uwezo wa kutumia teknolojia ili kuhimili ushindani wa kikanda na kimataifa. Amesema Serikali itaendelea kuboresha sera, sheria na mifumo ya mafunzo ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana.
Awali, akitoa salamu za wananchi wa Dodoma, Mkuu wa Mkoa huo Rosemary Senyamule ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutenga bajeti maalum kwa ajili ya mafunzo ya uanagenzi, akisema hatua hiyo inaonyesha uwekezaji katika rasilimali muhimu ya Taifa, hususan vijana. SOMA: Vijana Kagera wapewa elimu mikopo ya halmashauri
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu), Zuhura Yunus, amesema Serikali kupitia ofisi hiyo inatekeleza Mafunzo ya Uanagenzi kupitia Programu ya Taifa ya kukuza ujuzi nchini tangu mwaka wa fedha 2016/17. Amesema lengo la programu hiyo ni kukuza ujuzi wa nguvukazi iliyopo katika soko la ajira ili kuongeza tija katika uzalishaji wa bidhaa na utoaji wa huduma.
Naye Mkuu wa Chuo cha Don Bosco Dodoma, Mhandisi Dkt. Justine Mulebya, ameishukuru Serikali kwa kukipatia chuo hicho wanafunzi 650 na kuiomba iwezeshe wahitimu wa mafunzo ya uanagenzi kwa vifaa ili waweze kujiajiri na pia kuajiri vijana wengine baada ya kuhitimu.




hі!,I rеally like your writing so much! proportion we Ьe in contact moгe aЬout
your post on AOL? I гequire a specialist on this space to solve
my problem. May be that is you! Having a look forward
to peer you.
my web blog … digital banking
Hi! Do you know if they make any plugins to safeguard against
hackers? I’m kinda paranoid about losing everything
I’ve worked hard on. Any tips?
I have been exploring for a little for any high-quality articles or blog posts on this sort
of area . Exploring in Yahoo I at last stumbled upon this web site.
Reading this information So i’m happy to convey that I have an incredibly good uncanny feeling I came
upon just what I needed. I so much for sure will make sure to don?t forget this website and
provides it a look regularly.
Excellent post. Keep posting such kind of info on your
site. Im really impressed by your blog.
Hello there, You have done a fantastic job.
I will certainly digg it and in my opinion suggest to my friends.
I am sure they will be benefited from this web site.