Mkandarasi aelekezwa kuongeza kasi ujenzi stendi

SINYANGA: MKANDARASI aliyepewa kazi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa stendi mpya ya mabasi ya Katunda mkoani shinyanga ameelekezwa kuongeza kasi ya utekelezaji ili mradi uweze kukamilika na kutoa hudu kwa wakati.

Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi an Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCMA, Kenani Kihongosi ametoa agizo hilo leo Machi 6,2026 alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Amesema kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa ni kwamba mradi huo unatakiwa kukamilika kufikia Oktoba mwaka huu, akieleza kuwa hakuona mapungufu katika majengo kwa sababu yamejengwa kwa ubora.

Akisisitiza pamoja na na changamoto hizo bado mkandarasi anatakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji hata ikimbidi kuongeza vifaa ili mradi uwe tayari ufikapo muda elekezi wa mkataba.

“Mradi huu mkandarasi mmeujenga vizuri lakini muongeze kasi tunachohitaji mradi ukamilike hatuhitaji kuona majengo tunataka ukamilike ili huduma zianze tutolewa,” amesema kihongosi.

Pia ameelekeza kuhakikisha vibarua wanaofanya kazi katika mradi huo kulipwa stahiki zao kwa wakati, akieleza kuwa hajaambiwa lakini ni wazi kuwa hawajalipwa hivyo alitaka walipwe kabla hajaondoka mkoani humo.

“Hapa kuna jambo la vibarua hamjanipa taarifa lakini inaonekana vibarua wanadai walipwe malipo yao haraka na ikiwezekana walipwe kabla sijaondoka katika mkoa huu wa shinyanga Mkuu wa Mkoa simamieni haki za watu watu walipwe watu wanapofanya kazi kwa furaha,” amesisitiza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mhandisi Mshauri wa Serikali, Emmanuel Kasimba mradi huo umekamilika kwa asilimia 35 ambao ni moja ya miradi inayotekelezwa katika kifurushi kimoja kwa kiasi cha Sh bilioni 26.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button