Shinyanya kuwa kitovu uchumi kanda ya ziwa

SERIKALI ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha Mkoa wa Shinyanga unakuwa kitovu cha uchumi katika Kanda ya Ziwa.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amesema hayo leo Machi 6,2026 alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege uliojengwa Kata ya Ibadakuli Mkoani Shinyanga.

Akizungumza baada ya kukagua uwanja huo Kihongosi amesema kama chama wameridhishwa na utekelezwaji wa mradi huo akiwaeleza kuwa hayo yote ni mapenzi makubwa ya Rais Samia kuhakikisha Shinyanga inakuwa ni kitovu cha uchumi katika kanda ya ziwa.

Amesema kutokana na kazi na upendo huo mkubwa wananchi wanawajibu wa kushirikiana na serikali kumuombe Rais nakulinda miundombinu na kuendelea kudumisha umoja upendo na amani katika maeneo yao.

Pia amempongeza Meneja wa Wakala wa barabara Nchini (TANROADS) kwa kufanya kazi kwa ubora stahiki na uaminifu mkubwa hali inayosaidia kuimarisba imani ya wananchi kwa serikali yao.

“Tukifanya kazi kwa ubora wa namna hii watanzania watajenga imani kubwa na serikali yao lakini tukifanya tofauti watanzania watakasirika na kwenda kwa chama na chama hakitovumilia watumishi wazembe,” amesema Kihongosi.

Awali, Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Meneja Tanroads, Mhandisi Ntuli Mwaikokesya ilielezwa mradi huo umegharimu zaidi ya Sh bilioni 44, ulianza kutekelezwa Aprili 4,2023 na umefikia asilimia 94.7 ya utekelezaji wake na mkandarasi wake ni China Henan International Cooperation Group Co. Ltd.

Alisema kwa tathmini ya kitaalamu iliamuliwa kuongeza urefu wa njia ya kuruka na kutua ndege hadi mita 2,200 badala ya mita 2000 ya awali, ili kuwezesha kiwanja hicho kuhudumia kwa usalama ndege za Serikali na za kibiashara za aina ya Bombardier Q400.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button