Serikali yapewa kongole ulinzi haki za watoto

MOROGORO: Serikali imepongezwa kwa kuendelea kuongeza juhudi katika kulinda haki za watoto pamoja na kuimarika kwa usajili wa vizazi na mifumo ya ulinzi wa mtoto.
Pongezi hizo zimetolewa na Shirika la Save the Children Tanzani kupitia Mkurugenzi wake, Angela Kauleni mbele ya Mkurugenzi wa Wizara ya Katiba na Sheria, Kamishna Neema Mwanga.

Kamishna Mwanga alimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, Dk Juma Homera katika ufunguzi wa kikao cha uhakiki wa ripoti ya Asasi za Kiraia (UPR -Universal Periodic Review) mzunguko wa nne , kilichofanyika mjini Morogoro.
Kauleni amesema kuendelea kwa Serikali kuongeza juhudi hizo kumewezesha kupungua kwa ukatili dhidi ya watoto kwa asilimia 26.5 kwa mujibu wa ripoti ya (Voilence Against Children Survey in Tanzania (VACYS 2024).

Ametaja mafanikio mengine ni utekelezaji wa Mwongozo wa mwaka 2022 unaowawezesha wasichana waliopata ujauzito kurejea shuleni na uimarishaji wa huduma za kijamii kupitia programu za ulinzi na ustawi.
“ Hatua hizi zinadhihirisha dhamira njema ya Serikali kujenga msingi thabiti kwa ustawi wa mtoto” amesema Kauleni.
Mkurugenzi wa shirika hilo amesema pamoja na mafanikio, bado zipo changamoto ambazo zinahitaji mwitikio wa pamoja, akibainisha ni pamoja na uhaba wa Maofisa Ustawi wa Jamii wanaohitajika kushughulikia masuala ya Watoto katika jamii.
“Wote tunafahamu kwamba kiwango cha mahitaji katika jamii ni kikubwa kuliko uwezo wa mfumo uliopo,”alisema Kauleni.
Kauleni ametaja eneo lingine ni sheria zilizopitwa na wakati na baadhi ya vifungu, hasa vinavyoathiri wasichana ikiwemo vinavyohusiana na ndoa za utotoni na vinahitaji marekebisho ya haraka.
Mbali na hayo amesema zipo changamoto mpya za karne ya sasa hususan ukatili wa kimtandao, madhara ya mabadiliko ya tabianchi, na biashara haramu ya binadamu vinaendelea kuongeza hatari kwa watoto.
Kauleni amesema dhamira ya Save the Children kuwa itaendeleakushirikiana naSerikali na wadau wote katika kuimarisha mifumo ya ulinzi wa mtoto, kusukuma mbele ajenda ya elimu jumuishi, na kusaidia ushiriki wa watoto katika maamuzi.
Ametaja eneo lingine ni kuwekeza katika programu zinazoimarisha ustawi na mustakabali wa mtoto ,kusimama na wadau wengine katika kutafuta suluhisho la marekebisho ya sheria kama za kuondoa ndoa za utotoni, kuondoa ukatili wa kuchapwa viboko.
“Mtoto anayelelewa katika mazingira salama leo, ndiye raia mwadilifu, kiongozi wa kesho, na nguvu ya uchumi wa baadaye wa Taifa letu” amesema Kauleni.
Kwa upande wake Kaimu Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Haki Binadamu Tanzania (THRDC) ,Wakili Halima Sonda amesema Mtandao huo unatambua hatua chanya zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika baadhi ya maeneo .
Amesema miongoni mwa maeneo ni maboresho katika utoaji wa huduma za afya na hatua zinazoendelea katika kuanzisha mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote, na mageuzi ya sera yanayolenga kuimarisha usawa wa kijinsia na elimu jumuishi.
“ Lengo la mchakato wa UPR si kulaumu tuu bali ni kutoa fursa ya majadiliano ya kujenga yatakayoisaidia nchi katika kuendelea kuimarisha ulinzi na haki za binadamu kwa kuzingatia Ushahidi na mapendekezo yanayotekelezeka,”amesema Sonda.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com