DC Handeni ataka umoja, mshikamano

TANGA: MKUU wa Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Salum Nyamwese, amewataka wananchi wa wilaya hiyo kudumisha mshikamano na utamaduni wa kusaidiana, huku akiongoza harambee maalum ya kuchangia makundi yenye uhitaji kuelekea sikukuu ya Eid al-Fitr.

​Katika hafla hiyo ya Iftar iliyoandaliwa na ofisi yake na kuwakutanisha viongozi wa dini, serikali na wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batilda Burian, ameunga mkono juhudi hizo kwa kuchangia Sh milioni 1 kusaidia wenye mahitaji.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, DC Nyamwese alisema lengo la kukutana na kufuturu pamoja ni kuimarisha uhusiano kati ya viongozi na wananchi, sambamba na kuwakumbusha wenye nacho wajibu wao wa kuwajali wasiojiweza.

​”Mshikamano na umoja wetu ndio msingi mkuu wa amani na maendeleo tuliyonayo Handeni. Ni muhimu kila mmoja akaguswa kusaidia makundi maalum kama yatima, wazee na watu wenye ulemavu ili kuimarisha ustawi wa jamii yetu,” alisema DC Nyamwese.

​Mapema kabla ya kuanza kwa hafla hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya alitembelea Gereza la Wilaya ya Handeni ambapo alitoa msaada wa bidhaa mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu.

​Alibainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuonyesha upendo na kuwafanya wahusika wajione kuwa ni sehemu ya jamii, hususan katika kipindi hiki cha kuelekea kilele cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na sikukuu ya Eid.

Viongozi wa dini waliohudhuria hafla hiyo walipongeza hatua ya DC Nyamwese kwa kuunganisha jamii na kusema kuwa vitendo hivyo vya huruma ni fundisho tosha la imani na utu.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

  3. Many people in the United States and other parts of the world have lost their regular occupations. This was terrible, and I understand how you felt when you had no money left for your family. But I’m here to give a simple method that will fix all of your money issues right now. Working from home might earn you more than $15k each month simply by remaining at home. So, for further information, go to this website immediately and start earning right away………..

    GOOD LUCK. ==-…………………………….-=>>) https://earnsmartwithus.netlify.app/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button