Serikali yadhamiria wananchi kupata makazi bora, nafuu

 

DAR ES SALAAM: Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameeleza dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania hususan vijana, wanapata makazi bora na ya gharama nafuu kupitia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Majengo (TBA).

Ulega ameyasema hayo jijini Dar es Salaam mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati ilipotembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi wa umma katika eneo la Magomeni Kota Awamu ya Pili pamoja na nyumba za makazi za Canadian Village zilizopo Masaki.

Amebainisha kuwa hadi sasa jumla ya nyumba 174 zinaendelea kujengwa katika eneo la Temeke jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusaidia vijana kupata makazi ya gharama nafuu na hivyo kupunguza changamoto ya uhaba wa nyumba katika jiji hilo.

Aidha, Ulega amesema maono ya Rais Samia ni kuhakikisha miradi ya aina hiyo inatekelezwa pia katika majiji mengine nchini kulingana na mahitaji yaliyopo, ikiwemo Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma.

Katika ukaguzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso, amesema kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo baada ya kufanya ukaguzi na kubaini kuwa ujenzi unaendelea kwa viwango vinavyokubalika na vya kisasa.

Amesema ubora wa nyumba hizo unatokana na ufuatiliaji mzuri unaofanywa na Wizara ya Ujenzi pamoja na Wakala wa Majengo (TBA) katika kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo.

Naye, Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro amesema ujenzi wa mradi wa Magomeni Kota Awamu ya Pili uliofikia asilimia 65 unahusisha majengo matano ya makazi yenye sakafu nane, ambapo kila jengo lina uwezo wa kuchukua familia 16 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2026.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. Google paid $200 a hour on the internet..my close relative has been without labor for nine months and the earlier month her compensation check was $51005 by working at home for 10 hours a day….. E­v­e­r­y­b­o­d­y m­u­s­t t­r­y t­h­i­s j­o­b n­o­w b­y j­u­s­t u­s­e ­t­h­i­s

    GOOD LUCK.:) http://www.giftpay7.vip

  2. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  3. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

  4. This was a really unshaky mood gummies cbd thc . The devices felt secure, the pour was cagey flatten, and there weren’t any annoying clogging issues, which makes a huge difference. The flavor stayed bathe a exhaust and enjoyable without starting to bit burnt too with dispatch, and the cart itself looked well made morality revealed of the box. The total hither it felt consistent and easy to use. For anyone looking for a straightforward cart with considerate flavor and dependable ironmongery, this at one definitely checks the boxes.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button