Watoto kupewa chanjo ya polio Shinyanga

SHINYANGA: WATOTO wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi 10 mkoani Shinyanga wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Polio ili kuwazuia kupata virusi vya ugonjwa huo nakuweza kuwaepusha na ulemavu wa kudumu au vifo.

Hayo yamesemwa leo na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Yudas Ndungile alipokuwa akifungua kikao na waandishi wa habari huku akieleza kampeni ya uzinduzi wa kutoa chanjo ya polio itaanza rasmi tarehe 24 hadi tarehe 27 mwaka 2026 kupitia vituo vya afya, nyumba kwa nyumba,vituo vya kulelea watoto mchana (Daycare)pamoja na shuleni.

“Wazazi watatakiwa kuwapeleka watoto hao ambao ni walengwa kwani mkoa huu unatarajia kuwafikia watoto takribani 781186 ambapo utafiti uliofanyika jijini Mwanza umeonyesha maji taka yanavimelea vya virusi vya polio na serikali ikaona kuwapatia chanjo watoto hao ili kuweza kuwanusuru na ulemavu wa kudumu au vifo,”amesema Dk Ndungile.

Dk Ndungile amesema kampeni hiyo itafanyika kwenye mikoa ya kanda ya ziwa ambayo ipo kwenye hatari ya vimelea kusambaa nakuwa hatari kwa watoto na serikali kuona ni vyema kuanza kuzuia kwa kuwapatia chanjo mapema kuweza kuzuia kabla ya kupatikana kwa madhara makubwa.

“Takwimu hizi zimechakatwa na NBS kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kulingana na maeneo husika ambapo kila Halmashauri zitatoa chanjo ya polio kwa watoto hao ikiwa Halmashauri ya Ushetu watoto 148,557, Kahama Manispaa 145,820, Msalala 138,172, Kishapu 120,130, Halmashauri ya Shinyanga 166,428 na Manispaa ya Shinyanga 62,192,” amesema Dk Ndungile.

Mratibu Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa wa Shinyanga Moses Mwita alisema ugonjwa wa polio umekuwa tishio kwa miaka mingi ambapo nchini Tanzania kwa mara ya mwisho mtu aliyegundulika na ugonjwa huyo ni mwaka 1996 hivyo serikali imekuwa ikitoa chanjo hii kwa watoto wenye umri tofauti tofauti baada ya kuzaliwa.

Mwita amesema chanjo ya polia baada ya kampeni kuanza mwezi huu itatolewa kwa njia ya matone siyo Sindano na watapita wataalamu kwenye kila nyumba kuanza kuhamasisha lengo watoto waliokusudiwa wapate chanjo hiyo ni bure na haina madhara yoyote.

“Chanjo hiyo imelengwa kwa mikoa saba ambayo ni Mwanza,Singida,Mara,Tabora Simiyu,Geita na Shinyanga baada ya Kuzindua ngazi ya mkoa kila Halmashauri nazo zitafanya zoezi hilo nakuwafikia watoto walilengwa na tayari wataalam wamepatiwa maelekezo zaidi amesema Mwita.

Mtoa Elimu kwa Umma Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya, Anne Shuma amesema waandishi wa habari wanategemewa kuhamasisha na kufikisha ujumbe kwa wananchi ambapo hakuna mgonjwa wa polio wala mlipuko wa polio lakini kuna vimelea na sasa serikali imeanza kuchukua tahadhari kuwawekea kinga hata kama alikwisha chanjwa atarudia tena.

“Watoto hawa wengi watakuwa shuleni na nyumbani na chanjo hizi zitatolewa bure serikali imegharamikia ndiyo maana haziuzwi maeneo yoyote hivyo wazazi wajitokeze kuwalinda watoto na zoezi litazinduliwa kwenye mikoa hiyo kitaifa litazinduliwa mkoani Mwanza na Waziri wa Afya,”amesema Shuma.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button