Serikali yawekeza trilioni 6 barabara,madaraja

SERIKALI imeongeza kasi ya uwekezaji katika miundombinu ya barabara na madaraja nchini, ikiwekeza zaidi ya Shilingi trilioni 6 katika miradi mikubwa 79 inayoendelea kutekelezwa, hatua inayolenga kuchochea ukuaji wa uchumi, kurahisisha usafiri na kuimarisha biashara za ndani na kikanda.
Akizungumza leo Machi 30, 2026, jijini Dodoma, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Elphatar Mlavi, alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jumla ya kilomita 5,769.74 za barabara zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji, ambapo kilomita 1,495.45 zimekamilika kwa kiwango cha lami huku kilomita 3,677.67 zikiendelea kujengwa.
Amesema hadi Desemba 2025, mtandao wa barabara nchini umefikia kilomita 182,164.41, ambapo kilomita 37,734.41 ni barabara za kitaifa zinazosimamiwa na TANROADS. Kati ya hizo, asilimia 87 zipo katika hali nzuri au ya wastani, mafanikio yanayoonesha juhudi za Serikali katika kulinda uwekezaji wa miundombinu hiyo muhimu.

Kwa upande wa miundombinu mikubwa, TANROADS imekamilisha ujenzi wa madaraja makubwa nane, ikiwemo Daraja la J.P. Magufuli na Tanzanite, huku madaraja 17 yakiendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini ili kuboresha mawasiliano na usafirishaji.
Katika hatua nyingine, Serikali imeendelea kuimarisha udhibiti wa uzito wa magari kwa kuongeza vituo vya mizani na kutumia teknolojia ya kisasa ya kupima magari yakiwa kwenye mwendo hatua inayolenga kulinda barabara dhidi ya uharibifu wa mapema na kuongeza uwazi katika usimamizi.SOMA: Bajeti barabara MUHAS kutua bungeni, kamati yatoa maagizo
Hata hivyo, TANROADS imeeleza kuwa inaendelea kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, ukuaji wa kasi wa miji na kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi. Pamoja na hayo, imeweka mikakati ya kutumia teknolojia mbadala, kujenga miundombinu himilivu na kuongeza ushiriki wa wazawa katika miradi ya ujenzi ili kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kuwa mhimili wa maendeleo ya taifa.



JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com