Lufingo: Tulinde amani ya nchi

MSANII wa filamu za Bongo Movie, Daniel Lufingo, amesema kuwa uwepo wa amani katika jamii ni jambo la msingi kwa wasanii kwani kazi zao hutegemea mazingira tulivu pamoja na ushirikiano mzuri kati ya jamii na serikali.

Akizungumza na Habari Leo, Lufingo maarufu kama “Adam” kupitia tamthilia ya (Noma), amesema kuwa amani ya kweli hujengwa juu ya msingi wa haki, ambapo kila mtu anapaswa kutimiza wajibu wake kwa manufaa ya jamii.

Amesema kuwa sekta ya sanaa inahitaji mazingira salama na tulivu ili wasanii waweze kuibua ubunifu wao na kutoa kazi zenye tija kwa jamii. “Amani ni tunda la haki. Bila haki, haiwezekani kuwa na amani ya kudumu,” alisema Lufingo. SOMA: Vijana wataka amani ilindwe

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button