Chatanda aahidi mchango wake sekta ya afya

DODOMA: Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa (UWT), Mary Chatanda ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Hospitali Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, amesema kuwa ataendelea kutoa mchango wake wa kitaalamu na wakiuongozi katika kuhakikisha huduma za afya mkoani humo zinazidi kuimarika kwa manufaa ya wananchi wote.

Chatanda ameyasema hapo aliposhiriki kikao cha Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital) kilichofanyika leo Aprili 15, 2026.

‎Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuboresha miundombinu ya hospitali, kuimarisha upatikanaji wa vifaa tiba pamoja na kuongeza ufanisi wa watumishi wa sekta ya afya ili kuhakikisha huduma bora, salama na kwa wakati zinawafikia wananchi.

‎Hata hivyo amebainisha kuwa ushirikiano kati ya wadau mbalimbali wa sekta ya afya ni muhimu katika kufanikisha jitihada za kuboresha huduma hizo.
‎-

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button