Wanafunzi wapigwa msasa elimu matumizi ya bima

DAR ES SALAAM: WADAU wa sekta ya bima nchini wameendelea kutoa elimu kwa wanafunzi kupitia mashindano ya “Bima Debate” yaliyoandaliwa ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya Siku ya Bima yatakayofanyika kuanzia 26/06/2026 jijini Arusha.

Mashindano hayo yamewakutanisha wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na vyuo vikuu mbalimbali kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa bima katika maisha ya kila siku.

Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania Kanda ya Mashariki, Zakaria Muyengi, amesema sekta ya bima bado inahitaji elimu kubwa kwa jamii ili wananchi wengi zaidi waweze kuelewa faida zake na kushiriki kikamilifu katika huduma hizo.

Muyengi, ambaye alikuwa Jaji Mkuu wa mashindano hayo pamoja na mgeni rasmi, amesema wanafunzi wakipewa elimu ya bima mapema huwasaidia kujenga uelewa wa kudumu kuhusu namna huduma hiyo inavyoweza kusaidia kulinda maisha, biashara na mali dhidi ya changamoto mbalimbali.

Amesema hatua ya kuwafikia wanafunzi mashuleni ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuhakikisha kizazi kijacho kinakuwa na mtazamo chanya kuhusu sekta ya bima ambayo inaendelea kukua kwa kasi nchini Tanzania.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa maandalizi ya mashindano hayo, Esther Mwamengo, amesema jamii bado ina dhana potofu kuhusu huduma za bima kutokana na ukosefu wa elimu sahihi, hali inayochangia wananchi wengi kushindwa kuona umuhimu wake.

Mwamengo amesema wanafunzi waliopata elimu hiyo wanatarajiwa kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha matumizi ya bima katika familia zao na jamii kwa ujumla, huku akisisitiza kuwa elimu ndiyo msingi wa kukuza sekta hiyo hapa nchini.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..    https://www.work27.info

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button