BOT yahimiza wakulima kuchangamkia mikopo ya riba nafuu

DODOMA: BENKI Kuu Tanzania (BOT) imewahimiza wakulima kuchangamkia mikopo ya riba nafuu inayotolewa na mabenki nchini kupitia fedha za Mfuko wa Shilingi trilioni moja ulioanzishwa na Benki hiyo mwaka 2021.
Akizungumza katika Maonesho ya 88 katika Viwanja vya Dk John Malecela, Mchumi wa BOT Caritas Chawene alisema, mfuko huo umeleta mafanikio makubwa kwenye sekta ya kilimo.
“Mfuko huu ulioanzishwa mwaka 2021 kwa kutenga Sh trilioni moja, kwa ajili ya kukopesha mabenki kwa asilimia tatu na mabenki kukopesha wakulima kwa riba ya chini ya asilimia 10,” alisema.
Benki za CRDB, TADB, TCB na NMB zimekuwa zikitoa mikopo hiyo kwa wakulima nchini baada ya kukidhidhi vigezo vya kutokuwa na mikopo chechefu inayozidi asilimia tisa na benki hizo kuwa hai na kuendelea kutoa huduma.
Tangu BOT imeanzisha mfuko huo na benki kuanza kukopesha wakulima, kumekuwa na ongezeko la uzalishaji kwenye sekta ya kilimo kutoka asilimia 2.3 mwaka 2021 hadi asilimia 13.7 mwezi Juni 2026.
Takwimu zinaonesha kwamba hadi mwaka huu, benki zimetoa mikopo inayofikia asilimia 40 na imechangia sana katika kukuza sekta ya kilimo.
Wakulima wametumia fursa hiyo ya kukopa mikopo kwenye mabenki kwa riba nafuu na wametumia mikopo hiyo kuongeza uzalishaji mazao mbalimbali.
Pia amewata wauzaji wa pembejeo na wazalishaji wengine wasisite kufika kwenye mabenki mbalimbali kupata mikopo hiyo yenye riba nafuu na inaleta maendeleo kwa nchi.
Caritas alisema, mfuko huo upo hai na unaendelea kutoa mikopo kwa wakulima, hivyo anawahimiza wakulima na vikundi mbalimbali kwenda kukopa fedha kwenye mabenki kwani bado zipo.
Kuanzishwa kwa mfuko huo, wa Sh trilioni moja kumeleta faida kubwa pamoja na kuongeza uzalishaji mazao, pia kumeongeza mitaji na kuzalisha ajira kwa wakulima nchini.
BOT imekuwa ikifuatilia utoaji wa mikopo hiyo kwenye mabenki kama zinakopesha wakulima kwa kuzingatia vigezo.




There is some obstacle to get such loan especially CRDB bank most of bank officer they don’t want to provide such loan on time also ,not all farmers benefits from that loan we end upo Lossing our time and transport fees to ask for that loan