Matatani wakidaiwa kukutwa na shehena ya mbegu zilizoibwa

MBEYA; JESHI la Polisi mkoa wa Mbeya limewakamata watu wawili kwa tuhuma za kupatikana na shehena ya mbegu za mahindi zilizoibwa,zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 56,mali ya Wakala wa Mbegu za Serikali(ASA).

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema watuhumiwa hao walikamatwa Septemba 20 jioni baada ya jeshi hilo kupokea taarifa kutoka kwa ASA ikieleza kuibwa kwa mifuko 375 ya mbegu za mahindi zenye ruzuku ya serikali yenye uzito wa tani zaidi ya 15.

Kamanda Kuzaga amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika Mtaa wa Viwandani, Kata ya Mwakibete, jijini Mbeya,wakiwa na shehena hiyo ikiwa imefichwa ndani ya ghala la kuhifadhia mizigo mbalimbali.

Jana Septemba 20 majira ya saa moja asubuhi,tulipokea taarifa ya kuibiwa mbegu hizo tulifanya ufuatiliaji na

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Ayubu Charles(36) na Meshack Mwashimala(48) wote wakazi wa Itewe,Mkoa wa Mbeya.

Habari Zifananazo

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button