Waziri Makonda kunguruma Dar kesho

DAR ES SALAAM; Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda kesho Septemba 24, 2026 anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zaituni Mkwama, imesema mkutano utaanza saa 4 asubuhi hoteli ya Hyatt, Dar es Salaam.
Mkwama amesema Waziri Makonda atazungumzia masuala mbalimbali yanayoihusu wizara hiyo ikiwemo matukio makubwa ya kitaifa na kimataifa yanayotarajiwa kufanyika nchini katika mwaka 2026/2027.
“Waandishi wa habari wote mnaalikwa katika mkutano huo, ambapo mtapata fursa ya kumuuliza Mhe. Waziri Makonda maswali mbalimbali, ambayo atayajibu papo hapo. Usajili wa waandishi wa habari utaanza saa 2:00 asubuhi hotelini hapo,” imesema taarifa hiyo.



