Patel atwaa ubingwa kwa mara ya tatu Afrika

MOROGORO: DEREVA mzoefu Karan Patel na mwongozaji wake Tauseef Khan wameweka rekodi nyingine kwa kuiwakilisha nchi yao kutwaa ubingwa wa Afrika kwa mara ya tatu wa Afrika Rally Championship katika mashindano ya  mbio za magari za Serengeti Rally of Tanzania.

Mahindano ya Serengeti Rally of Tanzania 2026 yamefanyika  kwa siku nne hadi 4,2026, kwenye  Shamba la Msitu la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS )mkoani Morogoro yakiwa ni  sehemu ya kalenda ya African Rally Championship na kushirikisha mataifa  ya  Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na Tanzania.

Patel akitokea kwenye timu ya Asas  amesema kufanikiwa kuwa bingwa kwa mara nyingine kumesababishwa na ushindani mkubwa aliopata kutoka kwa Mtanzania Manveer Baldi ambaye wanatokea timu Moja ya Asas.

“Ushindani mkubwa ulionekana katika hatua mbalimbali za mashindano na washiriki wakionesha umahiri, kasi na uzoefu katika kukabiliana na changamoto za njia za rally,” amesema Patel.

Patel amesema ushindani wa mwaka huu ilikuwa mkubwa kutokana na uboreshaji wa miundombinu ya barabara na kwamba  matamanio yake ni kushiriki mashindano makubwa zaidi licha ya kukabiliwa na changamoto ya gharama kubwa ya kushiriki mashindano ya kimataifa.

“ Licha ya kufanya vizuri kwenye  mashindano haya  na kutwaa ubingwa  kwa mara ya tatu fululizo , kitendo hiki kimeniongezea chachu kubwa ya kupiga hatuna zaidi  ya kutamani kwenda kushindana mashindano ya Dunia ya Magari” anasema Patel.

Naye mshindi wa pili wa Afrika Rally Championship, Manveer Bardi ambaye pia ni  mshindi wa kwanza kwenye National Rally Championship amempongezaPatel kwa ushindi alioupa kwani  uzoefu wake wa mashindano hayo ndio ilikuwa kikwazo kwake yeye kuibuka na ubingwa.

“Hii ni mara yangu ya nne kushiriki mashindano najitahidi kufanya vizuri , nimpongeze Patel ni mzoefu  sasa huu ni ubingwa wake  wa  mara tatu, nami sasa ninaniandaa kwa  mashindano yatakayofanyika mkoani Arusha, naimani nitafanya viziri,” amesema Bardi.

Katika mashindano hayo ,nafasi ya tatu ilinyakuliwa na Yasin Nasser kutoka timu ya Ampiano na wengine ni Ahmed Huwel kutoka timu Mkwawa akishika nafasi ya nne, nafasi ya Tano ikanyakuliwa na   Oscar Ntambila kutoka Uganda  na nafasi ya sita ilitwaliwa  na  Dk Nsereko Godfrey kutoka Uganda.

Kwa upande wake Dereva Susan Muwonge ambaye alikuwa ni mwanamke pekee na mwongozaji wake Musa Nsubuga kutoka nchini Uganda hakufanikiwa kumaliza mashindano baada ya gari aliyokuwa akiitumia kuharibika.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button