Mashabiki wapewa fursa mkakati kusaka vipaji

DAR ES SALAAM: MASHABIKI wa soka nchini wametakiwa kuwa sehemu ya msako wa vipaji kwa kupendekeza wachezaji wanaoamini wana uwezo wa kufika mbali, ikiwa ni sehemu ya msimu wa tatu wa Safari Lager Cup unaolenga kupata wachezaji 22 watakaounda kikosi kimoja.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu huo, Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Khensani Mkhombo, amesema watu walio karibu na soka katika jamii mara nyingi ndio wanaofahamu vipaji vinavyostahili kupewa nafasi kabla havijafahamika kwa kiwango kikubwa.
Amesema kupitia mpango wa ‘Maskauti Bingwa’, mashabiki watasaidia kuwaelekeza wataalamu kwenye wachezaji wanaoamini wanastahili kuonekana, huku tathmini na uamuzi wa mwisho ukifanywa na wataalamu wa ufundi wa soka.
Msimu huo tutatafuta wachezaji 22 wenye umri wa miaka 18 hadi 21 kutoka Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya, ambao watapata nafasi ya kushiriki katika Safari Lager Champions na baadaye kucheza dhidi ya Yanga Januari 30, 2027.
“Jumla ya timu 80 zitasajiliwa, timu 20 kutoka kila mkoa, usajili utaanza Oktoba 6 hadi 24, kabla ya bonanza la kwanza kufanyika Oktoba 25 katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
“Bonanza hilo litafuatiwa na Mwanza Novemba 7, Arusha Novemba 21 na Dar es Salaam Desemba 5, ambapo maskauti watapata nafasi ya kuwatathmini wachezaji katika mazingira halisi ya ushindani,” amesema.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com