Kamala Harris aondoka nchini kuelekea Zambia

MAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris ameondoka nchini baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kwanza barani Afrika.

Kamala aliwasili Tanzania Machi 29 akitokea Ghana ambako ndiko alianza safari yake ya siku tisa katika nchi za Afrika.

Anaelekea Zambia ambako atahitimisha ziara yake. Akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Kamala amesindikizwa na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango.

Akiwa Tanzania Kamala amezungumzia amezungumzia demokrasia, wanawake kupewa vipaumbele kwenye suala la uchumi na mambo mengine.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button