Lori lapoteza mwelekeo, laua bodaboda 10

WAENDESHA pikipiki ‘bodaboda zaidi ya 10, wamepoteza maisha katika Kaunti ya Migori nchini Kenya kufuatia ajali lori la kubeba mchanga kupoteza mwelekeo na kugonga kundi la bodaboda waliokuwa kando na barabara wakisubiri abiria.

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Migori Mark Wanjala alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema uchunguzi tayari umeanza kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Tukio limetokea leo asubuhi Aprili 8, 2023 huku ikielezwa kuwa  majeruhi  wamekimbizwa hospitali kwa matibabu.

Kwa mujibu wa mashuhuda dereva alipoteza mwelekeo katika barabara ya Migori – Isebania na baada ya hapo alianza kupiga kelele kuashiria hitilafu ya breki kabla ya ajali kutokea.

Walioshuhudia wamesema  kuwa watu wawili waliangushwa kwenye Mto Migori, huku juhudi za kuwaokoa zikiwa bado hazijafanyika kwani mto huo haufikiki kwa sasa.

Kwa mujibu wa raia mmoja aliyeshuhudia na kuzungumza na kituo cha habari cha TV47, breki za lori zilifeli na kuingia katika kundi hilo la bodaboda.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button