Sebastian Deo amchimba mkwara Yohana Daud

DAR ES SALAAM: Bondia Sebastian Deo Kutoka Mbande Chamanzi amemtangazia vita ulingoni mpinzani wake Yohana Daud kuelekea Pambano la safari ya Beach Oktoba 22, 2023 litakalofanyika Rongoni Beach Kigamboni Dar es Salaam

Akizungumza na Habari leo wakati akiendelea na maandalizi yake na mashabiki zake mtaani kwao amesema akiwa ulingoni anabadilika roho na kuwa mnyama mkali.

“Nitabadilika nitakuwa mnyama mkali nitamchakaza Yohana Daud mapema kwenye Pambano  siku hiyo.”amesema Sebastian.

Kwa upande wake shabiki wa masumbwi Sudi Hussen amesema bondia wake amejiandaa kuwaletea ushindi.

Naye Kocha wa Bondia huyo Abdallah Mtombo amesema wamejiandaa kumuunga mkono kwa kwenda kushuhudia akimtwanga TKO mpinzani wao siku hiyo kwa kuwa kajipanga kutembeza kichapo.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button