Mwankenwa kuzikwa leo Dar

DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Michezo Tanzania ambaye pia ni daktari wa klabu ya Azam FC, Mwanandi Mwankenwa anatarajiwa kuzikwa leo makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam baada ya sala ya alasiri.

Mwankenwa aliwahi kuwa daktari wa Taifa Stars, timu za Olimpiki, Michezo ya Afrika, Jumuiya ya Madola za Tanzania na JKT Ruvu kwa nyakati tofauti.

Alifariki juzi kwa tatizo la moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Azam FC, Zakaria Thabit ‘Zaka Zakazi amesema Mwankenwa atazikwa makaburi ya Kinondoni na maiti ataswaliwa Msikiti Mkuu wa Bakwata Kinondoni Dar es Salaam.

Daktari huyo amehudumu Azam FC kwa miaka 16 na aliingia katika udaktari michezoni mwaka 1982 akianza na timu ya JKT Ruvu.

 

Habari Zifananazo

Back to top button