Mpogolo ahimiza uangalizi malezi ya watoto

DAR ES SALAAM: MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amewataka wazazi kuzingatia na kuangalia mienendo ya watoto wanapokuwa majumbani ili iweze kuwasaidia kuwa na maadili shuleni na katika jamii kwa ujumla.
Mpogolo amesema hayo leo katika muendelezo wa ziara yake ya kutatua kero za wananchi wa Wilaya ya Ilala, alizungumza na wananchi wa kata tatu katika Jimbo la Segerea ambazo ni Buguruni, Mnyamani na Vingunguti.

Aidha, amesema kwa mujibu wa takwimu zinasema watoto wa kike ndio wengi ambao wameathirika zaidi na Ukimwi kuliko watoto wa kiume, hivyo aliwataka wazazi kuwatunza na kuwafunza maadiri mazuri watoto kwani atawasaidia kuepukana na vitu kama hivyo.
SOMA: DC Ilala zuieni rushwa
“Watoto wengi wanaathirika kwa mimba kutoka kwa watu wazima watoto wanapata ukimwi kutoka kwa watu wazima na sisi watu wazima wanaume tuwe na nidhamu tuwe na ustaarabu tujali malezi ya watoto,” amesema Mpogolo.

Alisema kama wazazi wakiwatunza vizuri kwani kukua katika maadili na malezi mazuri kutasaidia kuwalinxa kutokana na vitu viovu kama vibaka, pia alisema kwa kuzingatia hilo ni kutokuwaruhusu watoto kwenda kwenye vigoma kwani tabia zisizofaa wanajifunzia huko.
SOMA: Mpogolo: ‘Machinga’ zingatieni maelekezo
Pia aliwataka wananchi wa Kata hizo kuimarisha ulinzi shirikishi ili kusaidia kupunguza matukio ya wizi, unyang’anyi na ukabaji katika mitaa yao na kusaidia kuimarisha usalama wa wananchi.




